Sultan wa Oman, Qaboos bin Said Al Said ambaye anatajwa kuwa kiongozi aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi kwa nchi za Kiarabu amefariki dunia jana, Januari 10, 2020 akiwa na umri wa miaka 79.

Mahakama ya Oman imetoa taarifa ya kifo cha kiongozi huyo ikieleza, “kwa masikitiko makubwa na majonzi… tunasikitika na tunaomboleza kifo cha Mheshimiwa Sultan Qaboos bin Said, ambaye alifariki dunia Ijumaa.”

Ingawa haikuelezwa kwa haraka chanzo cha kifo chake, mwezi uliopita alirejea Oman akitokea nchini Ubelgiji alikoenda kwa ajili ya matibabu. Ripoti zilidai kuwa Sultan alikuwa anaumwa saratani.

Sultan huyo ameacha kitendawili cha urithi wa uongozi wake kwani alikuwa hajaoa na hakuwa na mrithi yoyote aliyepangwa au anayetarajiwa kutoka mikononi mwake.

Sultan huyo alimuondoa baba yake kwenye madaraka kwa kutumia mapinduzi akisaidiwa na Uingereza mwaka 1970. Kwa kutumia utajiri mkubwa wa mafuta alifanikiwa kuiletea Oman maendeleo makubwa yanayoonekana hadi leo.

Kwa mujibu wa utaratibu, Halmashauri maalum ya Kisultan inayoundwa na wanaume 50 inapaswa kukaa na kumchagua Sultan mpya ndani ya kipindi cha siku tatu tangu kiti cha Usultan kiachwe wazi.

Video: Bosi Nida anavyopitia katika tanuru la moto
Video: Umeya wa jiji Dar sasa kizungumkuti, Chadema waanza mwaka vibaya

Comments

comments