Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini nchini (SUMATRA) imeanza kutekeleza agizo la Rais John Magufuli la kujitathimini katika hali ya usalama kwa kuanzisha oparesheni ya ukaguzi wa leseni kwa madereva wa malori.
Ukaguzi huo wa leseni umefanyika katika kituo cha mizani Nala Manispaa ya Dodoma ukiendeshwa na Mwenyeti wa Bodi ya Wakurugenzi Sumatra Mhandisi Dkt. John Ndunguru na kusema kuwa zoezi hilo linafanyika maeneo mbalimbali nchini.
“Sumatra wameamua kufanya oparesheni hiyo kwa madereva wa malori kutokana na ajali ambazo zimekuwa zikitokea hususani kwa hivi karibuni katika maeneo mengi na kusababishwa vifo majeruhi na hasara wa mali,”amesema Dkt. Ndunguru
Hata hivyo, Dkt. Nduguru amesema ukaguzi huo wa zaidi ya magari makubwa 20 umefanywa kwa madereva ili kuangalia iwapo wana daraja E la leseni za udereva na iwapo kama wamepitia katika vyuo mbalimbali vya udereva vinavyotambulika na serikali.