Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye amepokonywa shamba lenye ekari 326 lililopo Mvumero mkoani Morogoro na kutakiwa kutokanyaga katika shamba hilo.
Sumaye amesema kuwa tukio hilo ni kisasi cha kisiasa ambacho hakiwezi kumradhimisha kurudi Chama cha Mapinduzi CCM, huku akiongeza kuwa yote anamwachia Mungu, kwani yeye hatakiweza.
“Kwangu mambo siyo mazuri, mtakumbuka baada tu ya kuingia upinzani Serikali ilitishia kuchukua mashamba yangu bila sababu za msingi, hata wakati wa kampeni baadhi ya viongozi wa CCM walitamka hadharani kuwa huyu dawa yake ni kumnyang’anya mashamba,”amesema Sumaye
Aidha, ameongeza kuwa Serikali imefanya uamuzi huo kwa madai kuwa shamba hilo halijaendelezwa kitu ambacho amekanusha kwa kusema siyo kweli kwani lina vitu mbalimbali ambavyo vimeendelezwa.
Hata hivyo, kwa upande wake, Waziri Mkuu aliyejiuzuru na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amesema kuwa suala hilo liko mahakani hivyo haina haja ya kulizungumzia.