Imeripotiwa kuwa Chelsea ilipangiwa mechi rahisi zaidi za mwanzo wa Ligi Kuu England (EPL) msimu huu ikiwa nafasi ya l4 kwenye msimanmo.
Vijana wa kocha Mauricio Pochettino walipambana kwenye ligi baada ya kushinda mechi moja na kufungwa mbili msimu huu.
Kwa mujibu wa takwimu za Opta, Chelsea imecheza mechi rahisi tano za mwanzo zaidi ya timu nyingine kwenye ligi.
Chelsea ilipata ushindi pekee dhidi ya Luton Town katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Stamford Bridge, Agosti, mwaka jana lakini tangu ushindi huo Blues ikafungwa dhidi ya Nottingham Forest nyumbani na kuambulia sare dhidi ya Bournemouth inayopambana kutoshuka daraja msimu huu.
Pia ilipokea kichapo kizito cha mabao 3-1 ilipocheza dhidi ya West Ham United, kipigo hicho kilikuwa cha pili baada ya Nottingham Forest.
Hiyo inamaanisha kwamba baada ya ushindi dhidi ya Luton na sare ya bao 1-1 dhidi ya Liverpool, klabu hiyo imekusaya pointi tano ikizidiwa 10 na vinara wa ligi hiyo, Manchester City.
Licha ya kuanza vibaya msimu huu, Supercomputer imeitabiria Chelsea kuimarika na itamaliza msimu ikiwa katika nafasi ya saba kwenye msimamo.
Hiyo inatosha kuirudisha Chelsea kwenye michuano ya Ulaya msimu ujao kwani itafuzu Europa au Conference League, kwa mujibu wa Supercomputer.
Mechi inayofuata ya Chelsea itakuwa dhidi ya Aston Villa iliyoanza kuimarika baada ya kuanza msimu kwa kusuasua.