Uongozi wa Azam FC umethibitisha taarifa za Kiungo Abubakar Salum ‘Sure Boy’ kutaka kuvunja mkataba na klabu hiyo, baada ya kugoma kurudi kambini kama alivyoamrishwa.

Sure Boy amegoma kurudi kambini, huku wachezaji wenzake Mudathir Yahya na Agrey Morris wakiitikia wito wa Uongozi wa klabu hiyo, baada ya kusitishiwa adhabu iliyokua ikiwakabili kwa zaidi ya miezi miwili.

Mkuu wa idara ya Habari na Mawasilino ya Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ amesema Sure Boy amegoma kurudi kambini hapo, huku akishinikiza mkataba wake uvunjwe.

“Aggrey Morris na Mudathir Yahya wamekubali kurejea mazoezini lakini Abubakar Sure boy amekataa, ameomba kuvunja mkataba na klabu ya Azam FC.”

“Uongozi utakaa na kuangalia uwezekano wa kukamilisha ombi lake, kwa sababu hili suala linawezekana na hakuna ambaye amedhamiria kumkomoa Sure Boy, haya ndio maisha ya soka.” amesema Zaka Zakazi.

Tetesi zinaeleza kuwa, Sure Boy huenda akajiunga na Young Africans katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la usajili, hatua ambayo imempa msukumo wa kushinikiza mkataba wake na Azam FC kuvunjwa.

Boxer kuondoka Young Africans, Adeyum kusubiri
Saido atamba Young Africans Bingwa 2021/22