Klabu ya Swensea City imemtupia virago kocha wake Garry Monk baada ya kushinda mchezo mmoja kati ya 11 ambayo ameingoza Swansea kwenye ligi ya England msimu huu.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 36 amekuwa kwenye kikosi hicho kwa zaidi ya miaka 11 akianza kama mchezaji lakini baadae mwaka 2014 akabidhiwa timu hiyo kama kocha mkuu akichukua nafasi ya Michael Laudrup.

Kipigo cha Jumamosi iliyopita cha magoli 3-0 dhidi ya Leicester City ulikuwa ndio mchezo wake wa mwisho kama kocha na amekiacha kikosi hicho kikiwa nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi.

Kocha huyo alijiunga na Swansea City kama mchezaji mwezi June mwaka 2004, akaisaidia Swansea kupanda daraja kucheza ligi kuu mwaka 2011 akiwa nahodha wa timu hiyo.

February 2014 aliteuliwa kuwa kocha wa muda lakini May 2014 akapewa nafasi hiyo kama kocha mkuu.

Mwezi August 2014 Swansea ilipata ushindi wa ugeni I dhidi ya Manchester United na huo ukawa ni ushindi wa kwanza kwa Swansea kwenye uwanja wa Old Trafford.

Swansea ilimaliza katika nafasi ya juu kwenye ligi msimu wa 2014-15 ikiwa nafasi ya nane kwa kufikisha jumla ya ponti 58.

Mexime: Mtibwa Sugar Tupo Kamili Kwa Muendelezo Wa VPL
Issoufou Garba Wa Yanga Atua Dar es salaam Kimyakimya