Klabu ya Swansea City, imeiweka kapuni ofa ya Pauni milioni 10 iliyokua inamlenga beki kutoka nchini Wales Ashley Williams, ambaye anatakiwa kwa udi na uvumba na klabu ya Everton.

Msemaji wa klabu hiyo ya Liberty Stadium, amethibitisha kukataliwa kwa ofa hiyo kwa kusema uongozi wa Swansea City hauna mpango wa kumuuza beki huyo wa katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

Everton wamepanga kumsajili Ashley kama mbadala wa beki kutoka nchini Engalnd John Stones, ambaye yu njiani kujiunga na Man City kwa ada ya pauni milioni 50, na tayari imeshaelezwa pande hizo mbili zimeshafikia makubaliano.

Hata hivyo tayari Ashley ameshaonyesha nia ya kutaka kuihama klabu hiyo, kufuatia kauli yale aliyowahi kuitoa mbele ya vyombo vya habari kwa kusisitiza suala la kutamani kucheza chini ya utawala wa Ronald Koeman.

Bado beki huyo mwenye umri wa miaka 31, hajajiunga na wenzake katika kambi ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi, kutokana na kuwa katika mapumziko baada ya kumaliza jukumu la kuitumikia timu yake ya taifa ambayo iliishia kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya Euro 2016.

Polisi wamtega Msigwa, wamruhusu kufanya mkutano hadi ‘Septemba Mosi’
Idrissa Gueye Arejeshwa Ligi Kuu Ya England (EPL)