Mfalme Mswati wa Swaziland ambaye hapo jana ameadhimisha miaka 50 ya uhuru wa nchi yake, ambapo ameipa jina jipya nchi ya Swaziland na kuita ‘eSwatini’
Ametoa taarifa hiyo kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo kutoka kwa Uingereza, na kusema kwamba nchi hiyo sasa itakuwa inaitwa eSwatini ikimaanisha ‘Sehemu ya Swazi’
Amefafanua kuwa mara nyingi mtu wa Swaziland akisafiri kwenda nchi za nje nchi yao hufananishwa na nchi ya Switzerland.
Aidha, kitendo hicho kimeonekana kutofurahiwa na baadhi ya watu wa Swaziland wakisema kuwa Mfalme alitakiwa kuelekeza nguvu kwenye uchumi wa nchi hiyo, na sio jina la nchi.
Hata hivyo, Jina la eSwatini lilishawahi kusikika likitamkwa na Mfame Mswati kwenye mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 2017, na kwenye hotuba yake alipokuwa akizindua Bunge la nchi hiyo mwaka 2014