Michuano ya kufuzu kucheza kombe la dunia mwaka kesho nchini Urusi imeendelea usiku wa jana ambapo mataifa mawili ya Croatia na Switzerland yamekata tiketi kwa ajili ya michuano hiyo.

Switzerland walitoka sale ya 0-0 na Northern Ireland matokeo ambayo yamewafanya kufuzu kuelekea kombe la dunia na hii ikiwa mara yao ya 4 mfululizo kwani mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Northern Ireland waliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Katika mchezo mwingine Croatia baada ya ushindi wa bao 4 kwa 1 dhidi ya Ugiriki siku chache zilizopita jana walitoka suluhu ya bila kufungana na Ugiriki katika mchezo wa marudiano na hivyo  kufuzu kucheza michuano ya kombe la dunia mwakani.

Croatia inakuwa timu ya 28 kufuzu kwa fainali za michuano hiyo na sasa kumebakia timu 4 tu kwa ajili ya kukamilisha idadi kamili ya wanaokwenda kushiriki kombe la dunia.

 

Askari waliobaka watoto wa miezi 18 wakalia kaa la moto
Majirani: Dk Shaka ‘Mnunuzi’ wa Majumba ya Lugumi ana roho ya kipekee