Omar Al Somah alifunga bao kupitia mkwaju wa penati dakika za mwisho na kuweka hai matumaini ya Syria kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018 kwa kutoka sare ya 1-1 na Australia.

Katika mchezo wao ya awali, mshambuliaji Al Somah alifunga bao dakika za mwisho dhidi ya Iran na kulazimisha sare na iliyowawezesha kumaliza katika nafasi ya tatu katika kundi lao la kufuzu kwa Kombe la Dunia kutokea bara Asia.

Alifunga bao hilo la kusawazisha Alhamisi nchini Malaysia – ambapo Syria huchezea michezo yao ya nyumbani – baada ya kuwa nyuma kutokana na bao la Robbie Kruse.

Mechi ya marudiano itachezwa Sydney Jumanne ijayo.

Mshindi atakutana na timu nyingine kutoka shirikisho la Concacaf kwenye mechi mbili (ya nyumbani na ya ugenini) kuamua timu itakayofuzu kwa Kombe la Dunia.

Video: Lema, Marsha watuma salamu kwa watu 'Wasiojulikana'
Andres Iniesta ajilipua FC Barcelona