Mhubiri maarufu kutoka Nigeria, T.B Joshua jana aliingia nchini akiwa na ujumbe muhimu na kupokelewa na rais mteule wa serikali ya awamu ya tano, Dkt. John Pombe Magufuli kisha kukutana na aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa.

Ujio wa T.B Joshua nchini unaaminika kuwa na lengo kuu la kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Dkt. Magufuli zitakazofanyika kesho ambapo watu wengine mashuhuri duniani pamoja na viongozi wa nchi mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria.

Muda mfupi baada ya kuwasili, mtumishi huyo wa Mungu aliyeambatana na mkewe, alifanya mazungumzo na Dkt. Magufuli na Mkewe Janeth na kisha kumtembelea Lowassa nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam.

TB Joshua na Lowassa Dar

Ni dhahiri kuwa, T.B Joshua alibeba ujumbe muhimu wa amani na maridhiano kwa ajili ya viongozi hao hususan katika kipindi hiki ambacho Lowassa ameendelea kupinga matokeo ya uchaguzi. Huenda ujumbe wa T.B Joshua utaweza kupenya moyo wa Lowassa na kukubali kuwa yaliyopita si ndwele.

T.B Joshua pia alipata nafasi ya kuonana na rais Jakaya Kikwete na kuzungumzumza.

TB Joshua na Rais Kikwete

Awali, T.B Joshua aliwahi kuwa mwenyeji wa Lowassa alipoenda Nigeria na kufanya ibada katika kanisa lake la The Synagogue Church of All Nations. Vivyo hivyo, Dkt. Magufuli na familia yake waliwahi kupata huduma ya maombezi kutoka kwa T.B Joshua.

Lowassa at SCOAN Nigeria

TB Joshua na Dkt Magufuli

Nani Anafuata Kupanda Kizimbani Baada Ya Yericco Nyerere?
'Hello' ya Adele Yavunja Rekodi Nyingine