Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limeiadhibu klabu ya Besiktas ya Uturuki kwa kuitoza faini faini, kufuatia kosa la taa za uwanja unaomilikiwa na klabu hiyo (Vodafone Arena), kuzimika wakati wa mchezo wa Europa League dhidi ya RB Leipzig ukiendelea mwezi uliopita.

Taa za uwanja wa Vodafone zilizimika kwa dakiika kumi kabla ya kuwaka tena na mchezo kuendelea.

UEFA wameitoza faini klabu hiyo faini ya Euro 25,000 sawa na dola za kimareiani 29,382.50.

Pamoja na hali kuwa tete upande wa taa, bado wageni RB Leipzig kutoka nchini Ujerumani walifanikiwa kuwabanjua wenyeji wao mabao mawili kwa sifuri, na kufanikiwa kuongoza kundi G.

Video: DC Mjema aingilia kati ugomvi wa FFU na wananchi jijini Dar
Ronald Koeman atoa neno la shukurani, aiombea kheri Everton