Zaidi ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Nyankumbu iliyopo Mkoani Geita, wamepatiwa mbinu za kuzingatia katika masomo yao, ili kukua kitaaluma na kuja kuwa watalaamu wa masuala ya madini baadae, ambapo wamejifunza mambo mbalimbali ikiwemo utafiti, uchimbaji, uendelezaji na usimamizi wa mazingira.

Wanafunzi hao wanaosoma mchepuo wa Sayansi, wamepatiwa elimu na uzoefu huo na Wafanyakazi wa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited – GGML, walipotembela banda la kampuni hiyo katika maoneosho ya sita ya teknolojia ya madini yanayoendelea kwenye viwanja vya Bombambili – EPZ, Mjini Geita.

Regina Mabula, Afisa Maendeleo ya uchumi wa jamii wa GGML, akiwapatia maelezo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Nyankumbu kuhusu mchoro wa 3D wa Uwanja wa Magogo ambao ni moja ya miradi inayofadhiliwa na GGML katika ujenzi wake.

Akizungumzia ziara hiyo, Meneja Mwandamizi anayeshughulikia mahusiano ya jamii GGML, Gilbert Mworia, mafunzo hayo yatawasaidia kujifunza na kupata uzoefu ikiwemo namna kampuni hiyo inavyoshirikiana na Serikali katika kutekeleza sera ya maendeleo ya jamii na kuzingatia sheria ya afya na usalama kazini.

Alisema, “GGML ni mdau muhimu pia katika masuala ya elimu hasa ikizingatiwa ndio iliyoanzisha na kusaidia maendeleo ya shule ya Sekondari ya Wasichana ya Nyankumbu ambayo sasa ni shule kubwa ya sekondari ya wasichana mkoani Geita iliyofunguliwa rasmi mwaka 2014.”

Israel Ryoba, Mtaalamu wa Usafi Kazini Idara ya Afya, Usalama, Mazingira na Mafunzo wa GGML akiwapatia maelezo wanafunzi wa shule ya sekondari Nyankumbu kuhusu sera za afya na usalama mahala pa kazi.

Aidha, Mworia aliongeza kuwa katika kampuni  hiyo ambayo pia ni mdhamini mkuu wa maonesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka mkoani Geita, imekuwa ikishiriki maonesho hayo kwa lengo la kuonesha ubunifu na mbinu bora za kisasa zinazotumiwa na kampuni hiyo kwenye sekta ya uchimbaji madini.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Uchumi wa Jamii GGML, Regina Mabula alisema, “tunathamini ushirikiano wetu na Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Nyankumbu na tunatarajia kuendelea kusaidia programu zao za elimu kwa sababu tunaamini kuwa kuwekeza katika elimu ni kuwekeza katika mustakabali wa maisha ya jamii yetu na nchi kwa ujumla.”

El-Cid Walter, Ofisa kutoka idara ya Usalama mahala pa kazi, HSE&T akiwaelezea wanafunzi wa shule ya sekondari Nyankumnbu mbinu za usalama zilizoiwezesha kampuni hiyo kushinda tuzo za afya na usalama mahala pa kazi.

Harusi yageuka msiba, mamia wafariki kwa Moto
Jipya laibuka bifu la Sancho, Ten Hag