Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amesema taaluma ya Uuguzi ni kazi ya uthubutu, utayari pamoja na kujitoa kwa ajili ya kuwahudumia wenye mahitaji ya kiafya huku akiwataka Wauguzi kuendelea kuchapa kazi kwa weledi na kwa kuzingatia miiko na maadili ya taaluma yao.

Kikwete ameyasema hayo wakati akizungumza na Wauguzi wa Mkoa wa Pwani kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani yaliyofanyika kimkoa katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze ambapo amewahimiza Wauguzi hao kuwahudumia wananchi kwa moyo na upendo wa hali ya juu.

Amesema, Serikali inatambua kuwa Wauguzi ni kundi muhimu sana kwani ndio shina na mhimili mkubwa wa utendaji na ufanisi wa sekta ya afya nchini na ulimwenguni kote.

Aidha, Kikwete ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka mazingira mazuri ya kufanyia kazi Wauguzi na kusema Ofisi ya Rais-UTUMISHI inaendelea kuzifanyia kazi changamoto za kimuundo za taaluma hiyo na changamoto nyingine itaishirikisha Wizara husika ya Afya ili ziweze kufanyiwa kazi.

Wanawake vaeni ujasiri msiogope changamoto - TAMWA-ZNZ
Serikali kuendeleza uimarishaji afya ya Mama, Mtoto