Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana mwishoni mwa wiki na kupitia kesi, mashauri mbalimbali kuhusiana na usajili na mikataba ya wachezaji na viongozi mbalimbali chini ya Makamu Mwenyekiti Wakili Mandi.

1. CHANGANYIKENI DHIDI YA POLISI DODOMA

Mchezaji Said Hamis Athumani

Kamati ilibaini kweli mchezaji Said Athumani Hamis alikuwa mchezaji wa Changanyikeni na taratibu za maongezi baina ya timu ya Polisi Dodoma na Changanyikeni kazikukamilika, hivyo kuwataka wakubaliane kuhusiana na fidia ya mchezaji kuhama kutoka Changanyikeni na baada ya maongezi Polisi Dodoma waliridhia kuwalipa Changanyikeni kiasi cha Shilingi 400,000/= kiasi ambacho kilikubaliwa pia na timu ya Changanyikeni.

Kamati imeitaka Sekretarieti kuandika barua Bodi ya Ligi kuifahamisha wawakate fedha kiasi cha shilingi 400,000/= (laki nne tu) timu ya Polisi Dodoma kwenye fedha watakazopewa na mdhamini.

 

2. PANONE DHIDI YA POLISI TABORA

Mchezaji Michael Chinedu

i. Kwa kesi ya tuhuma za mchezaji Mohamed Jingo kuwa sio raia wa Tanzania kamati imeona haina mamlaka ya kuthibitisha au kuamua uraia wa Mohamed

ii. Pia imeamua kujiridhisha kama ni kweli timu ya Polisi Jingo, TFF itaiandikia barua uhamiaji ili kupata uthibitisho wa uraia wa mchezaji husika haraka. Kamati imeamua kujiridhisha kama timu ya Polisi Tabora ilipata kibali cha Rais wa TFF kumtumia mchezaji Michael Chinidu bila ya kumlipia dola 2,000 kama kanuni zinavyoeleza.

 

3. MAWENZI MARKET FC DHIDI YA BURKINAFASO

Mchezaji Victor Mswaki

Baada ya kupitia kesi hii kamati ilijiridhisha kwamba klabu ya Burkinafaso Fc ilimsajili mchezaji bila ya kuwasiliana na klabu yake ya Mawenzi Market na yakwamba kanuni zinataka klabu inayotaka kumsajili mchezaji wa timu nyingine iwasiliane na timu inayommiliki mchezaji husika na kufikia makubaliano.

Kamati imeona timu ya Mawenzi Market wanayo haki ya juu ya mchezaji Victor Mswaki na hivyo kwa kuwa Burkinafaso FC iliongea kinyemela na mchezaji inatakiwa iilipe klabu ya Mawenzi Market na wamekubaliana kulipana kiasi cha Tsh 370,000/=.

 

4. KMC DHIDI YA AFRICAN LYON

Mchezaji Hamad Juma

Kamati imeona na imejiridhisha ya kuwa Hamad Juma Hamad ni mchezji halali wa African Lyon alisajiliwa kwa wakati na kwa kuwa usajili wake ulikubali kwenye mtandao wa mawasiliano hivyo hakukuwa na ulazima wa jina lake kuwekwa kwenye majina yanayohitaji pingamizi, hivyo kamati imejiridhisha

kwamba mchezaji Hamad Juma Hamad ni mchezaji halali wa African Lyon na imetupilia mbali malalamiko ya timu ya KMC na imetengua barua ya kumsimamisha kucheza aliyoandikiwa na TFF baada ya KMC kuleta malalamiko dhidi ya mchezaji huyo.

 

5. POLISI MOROGORO DHIDI YA BURKINAFASO

Mchezaji Victor Mswaki

Baada ya kupitia kesi hii kamati ilijiridhisha kwamba klabu ya Burkinafaso Fc ilimsajili mchezaji bila ya kuwasiliana na klabu yake ya Mawenzi Market na yakwamba kanuni zinataka klabu inayotaka kumsajili mchezaji wa timu nyingine iwasiliane na timu inayommiliki mchezaji husika na kufikia makubaliano.

Mswaki alisajiliwa na Burkinafaso ingawa TFF haikupewa taarifa sahihi vilevile halikuwekwa pingamizi lolote wakati wa usajili. Hivyo kwa mujibu wa kanuni 42(13) ya kanuni za Ligi daraja la kwanza kukitokea kasoro ya namna hiyo ya usajili klabu husika itatozwa faini ya Ths 500,000/= na matokeo ya uwanjani hayawezi kubadilishwa, kamati imeamua ya kwamba kwa kuwa shauri hili linafanana na shauri jingine na mchezaji husika ni yuleyule Victor Mswaki, hivyo klabu ya Burkinafaso haitaadhibiwa kwa kosa lile lile la mara mbili, na kamati imeonelea mchezaji aendelee kuichezea klabu yake ya Burkinafaso.

 

6. RHINO RANGERS DHIDI YA

Mchezaji Mohamed Jingo

Kamati haina mamlaka ya kuthibitisha au kutengua uraia wa mchezaji husika, hivyo Kamati imeitaka TFF iwaandikie barua uhamiaji kwa ajili ya kuchunguza uraia wa mchezaji Mohamed Jingo na mara kamati itakapopata uraia wa mchezaji husika itakaa kuliangalia suala hilo na kutoa maamuzi ya kesi husika.

 

7. LIPULI FC DHIDI YA KIMONDO FC KWA

Mchezaji George Mpole

Kamati ilijidhihirisha kwenye kikao chake cha mwisho cha tarehe 23 Desemba ilitoa zuio la mchezaji George Enock Mpole kuichezea Kimondo FC baada ya kupata barua ya pingamizi kutoka kwa Kurugenzi FC ikidai ni mchezaji wao halali na kwamba pamoja na taarifa za usajili kutolewa kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na press release namba 228 ambayo ilitolewa kwa vilabu vyote na vyama vya soka vya mikoa na kwenye vyombo vyote vya habari tarehe 24 Desemba bado klabu ya Kimondo pamoja na kupata taarifa za kutomchezesha mchezaji husika ilikaidi amri ya Kamati na kumchezesha mchezaji husika katika mchezo wao na Lipuli FC.

Aidha kamati ilipata pingamizi kipindi cha pingamizi baada ya usajili kufungwa tarehe 15 Desemba 2015, wiki ya tarehe 16-22 Desemba. Kwamba kamati imeona usajili ulifungwa tarehe 15 Desemba 2015, na kwamba tarehe 16 hadi 22 Desemba 2015 ni muda uliowekwa kwa ajili ya kuweka pingamizi. Katika muda huo klabu ya Kurugenzi ilileta pingamizi dhidi ya mchezaji George E. Mpole. Na kwamba kamati hii ilikaa tarehe 23/12/2015 pamoja na maamuzi mengine kamati iliamua kwamba klabu ya Kimondo FC isimchezeshe mchezaji husika yaani George Enock Mpole hadi watakapoelewana na Kurugenzi ya Mafinga na kwamba watakapokubaliana watatoa taarifa TFF ili TFF imruhusu mchezaji huyo aendele kucheza.

Na kwamba barua iliyowasilishwa na Kimondo mbele ya kamati hii kwamba walikubaliana tarehe 17/12/2015 haiwezi kuwa ushahidi mzuri kwa kuwa malalamiko yalikuwepo na kamati ilikaa tarehe 23/12/2015 na endapo kungekuwa na makubaliano katika hali ya kawaida kungekuwa na taarifa ambayo haikuwepo. Na kwamba hata baada ya taarifa rasmi kutolewa na TFF ya kwamba mchezaji amewekewa pingamizi na hatakiwi kucheza  hivyo wasimtumie mpaka wakikubaliana na klabu yake yaani Kurugenzi FC, hawakuwahi kutoa taarifa yoyote hivyo basi klabu ya Kimondo S.C imemchezesha mchezaji ambaye amesimamishwa na TFF.

 

Kanuni ya 42 (9) inasema kama ifuatavyo

“Timu yoyote ambayo itamchezesha mchezaji aliyechini ya adhabu ya kufungiwa /kusimamishwa au ambaye ametakiwa kulipa faini kwa maelekezo maalumu na hajalipakwa mujibu wa kanuni hii itapoteza mchezo huo na timu pinzani itapewa ushindi” Kwa mujibu wa kanuni hii kamati inatoa adhabu dhidi ya timu ya Kimondo SC katika mchezo uliochezwa tarehe 26/012/2015 dhidi ya Lipuli FC. Na kwamba timu ya Lipuli ndiyo itakuwa mshindi wa mchezo huu, hivyo itapewa pointi tatu (3) na magoli matatu (3).

Mchezaji huyo ataendelea kusimamishwa mpaka TFF itakapojiridhisha ya kwamba taratibu za usajili zimekamilika. Kurugenzi ndio itakayotoa taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya kamati.

 

8. BURKINAFASO FC DHIDI YA KIMONDO FC

Mchezaji Innocent Baru

Madai ya kwamba Burkinafaso Fc wanalalamikia kuwa mchezaji Innocent Boru Namwandu siyo mchezaji halali wa Kimondo SC na kwamba wanapinga matokeo ya mchezo yaliyotokea kwenye mchezo uliochezwa 2/01/2016 kati ya Kimondo SC na Burkinafaso na kwamba mfumo wa usajili wa TFF unaonyesha kuwa mchezaji huyo Innocent Boru Namwanda amesajiliwa na Kimondo SC na timu ya Kurugenzi FC haijawahi kuwasilisha barua wala kuleta pingamizi lolote TFF.

Kwa hiyo kamati inaona kuwa shauri hili au lalamiko hili halina ushahidi unaoweza kuthibitisha kuwa mchezaji huyo siyo mchezaji halali wa Kimondo SC. Na kamati imetoa uamuzi huo ikizingatia kwamba TFF ilitoa muda wa kuweka pingamizi lakini timu ya Kurugenzi FC inayosemekana ni mchezaji wao hawakuwahi kuleta pingamizi lolote mpaka sasa.

Kwa hiyo ushahidi uliopo kwa sasa ni kwamba Mchezaji husika ni mchezaji wa Kimondo SC ambaye usajili wake ulipitishwa na TFF.

 

9. MKAMBA RANGERS DHIDI YA WENDA FC

Mchezaji Vicent Costa

Kesi hii haikuwa na uwakilishi lakini kamati imeamua timu ya Wenda FC iwalipe mara moja Mkamba Rangers kiasi cha shilingi laki tatu (300,000/=) kama fidia ya kumpoteza mchezaji huyo.

Mchezaji anasimamishwa na timu za Wenda na Mkamba zitaandikiwa barua kufahamishwa kuhusiana na maamuzi ya kamati.

 

10. POLSII TABORA DHIDI YA AFRICAN SPORTS

Mchezaji Karim Humud

Klabu ya African Sports wameridhia kuilipa klabu ya Polisi Tabora kiasi cha Tsh 1,000,000/= toka kwenye vyanzo vyao vya mapato TFF/Bodi ya Ligi hivyo mchezaji Karim Humud Juma ameruhusiwa kuitumikia klabu yake ya African Sports kuanzia tarehe 15.01.2016.

 

11. AFRICA LYON dhidi ya Wachezaji

i. Morris Kaniki-Mwadui

ii. Miraji Athuman-Toto Africans na

iii. Emmanuel Simwanda-Mwadui

Kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji imeamua klabu husika ziandikiwe barua ya kumalizana na African Lyon na wapewe wiki mbili toka tarehe 15.01.2016 hadi tarehe 30.01.2016 kama watashindwa kumalizana watasimamishwa kuzichezea klabu hizo. Wakimalizana wapewe barua na African Lyon ndiyo itakayotuma barua TFF kuwaruhusu waendelee kucheza.

 

12. KESI MBALIMBALI ZA MADAI YA WACHEZAJI NA WALIMU

i. Kesi namba moja kati ya Fadhil Msemi anayewawakilisha wachezaji 28 wa KMC wanaodai malipo ya mishahara yao kwa mwajiri wao KMC

Kamati imeamua mwakilishi wa wachezaji ndugu Fadhil Msemi akae na viongozi wa KMC, katibu wao na mratibu wa timu wajadili na kupitia utaratibu wa malipo namna viwango vya malipo kwa wachezaji hao vinavyopaswa kuwa na iwasilishwe TFF Jumatatu.

ii. Kesi namba mbili ilikuwa kati ya Stand United dhidi ya wachezaji na wataalamu wake wanaoidai. Stand United iliwakilishwa na Ernest Brown kwa barua kwa hiyo maamuzi yote ya Kikao yatakuwa halali.

Kesi zilizojadiliwa zilikuwa ni kama ifuatavyo.

a. Kesi ya madai ya Mchezaji Peter Mutabuzi aliyeichezea Stand United dhidi ya klabu yake, Mutabuzi aliwakilishwa na kiongozi wa klabu yake ya sasa Frank Mchaki wa KMC.

Mchezaji huyu alikuwa anaidai klabu ya Stand United kiasi cha Tsh 3,400,000/= lakini kikao kilikubaliana alipwe kiasi cha Tsh 2,000,000/= ndani ya mechi nane za ligi toka tarehe ya kikao 15.01.2015.

b. Kesi kati ya Ndikumana Hamad dhidi ya Stand United, mwenyewe alikuwepo na pia aliwakilishwa na Fadhil Hussein. Ndikiumana anaidai klabu ya Stand malimbikizo ya mshahara, malazi na chakula kiasi cha shilingi 11,025,000/=. Wamekubaliana mchezaji anarudishwa kwenye klabu yake ya Stand United kuitumikia na pia madai yake watamalizana huko Stand na pia Stand imlipie gharama alizokuwa anaishi akiwa Dar es Salaam hotelini maana mchezaji sio raia wa Tanzania.

c. Ben Kalama ambaye alikuwa kocha wa makipa wa Stand United alikuwa anadai malimbikizo ya mshahara wake kiasi cha Tsh usd 1,350 aliwakilishwa na Fadhili Hussein yeye walikubaliana kuwa anarudishwa kwenye timu na watalipana huko huko madai yake. Kuhusu madai yake kiasi cha dola 1,350 kamati iliamua kwa kuwa ni madai halali na mwakilishi amekiri hilo basi wakatwe kwenye vyao vya mapato na TFF.

d. Mathias Lule dhidi ya Stand ya madai ya mishahara, posho na medical insurance kiasi cha Tsh 48,300,000/= aliwakilishwa na Fadhil Hussein. Ilikubaliwa ya kwamba alipwe kiasi cha usd 4,300.00 ambacho kimethibitishwa na kukubaliwa tayari na juu ya madai mengine watakaa na muajiri wake wa zamani na kuyajadili kuona namna ya kulimaliza suala hili. Fedha hiyo itakatwa kwenye vyanzo vyao vya mapato.

e. JAKI FOOTBALL ACADEMY dhidi ya Stand United kiasi cha shilingi 7,600,000. Jaki waliwakilishwa na Fadhil Hussein ambaye alisema deni wanaloidai Stand United ni kiasi cha Tsh 4,200,000/= na deni hili limekubaliwa na litalipwa na Stand United kwenye vyanzo vyao vya mapato toka TFF.

f. Muhibu Kanu dhidi ya Stand United anayeidai mishahara, na posho klabu ya Stand United kiasi cha Tsh 16,600,000/=. Makubaliano yamefikiwa kweli Muhibu anaidai Stand kiasi hicho na ameshaanza kulipwa kupitia Bodi ya ligi kiasi cha Tsh 2,600,000/= hivyo kiasi kilichobakia cha Tsh 14,000,000/= anaenda kujadiliana na muajiri wake kwa kuwa amerudishwa kazini.

g. Kesi kati ya aliyekuwa kocha msaidizi wa Stand United Emmanuel R. Massawe dhidi ya Stand United anayeidai Klabu ya Stand United kiasi cha Sh 12,100,000/= imehairishwa kwa kuwa muhusika hakuwepo wala hakutuma muwakilishi.

3. Kesi namba tatu ilikuwa ni kati ya Ndanda Fc dhidi ya wachezaji wake wanaoidai timu hiyo. Kesi hii ilishindwa kusikilizwa kwa kuwa wachezaji na wawakilishi wa wachezaji walikuwepo lakini klabu ya Ndanda FC haikutuma mwakilishi pamoja na kuletewa mwaliko siku ya tarehe 12/1/2016.

Hivyo kamati iliamua yafuatayo

a. Ndanda FC ikatwe kwenye vyanzo vyao vya mapato kiasi cha madai yaliyothibitishwa na mwakilishi wao katibu mkuu kwenye kikao kilichopita ambayo yalikuwa ya wachezaji wawili Rehani Kibingu kiasi cha tsh 2,000,000/= na Meshack Wilfredy Meshack aliyekuwa pia anadai kiasi cha Tsh 2,000,000/=.

b. Pamoja na katibu kuahidi kuleta ufafanuzi wa madai ya baadhi ya wachezaji tarehe 28.12.2015 kwa barua TFF mpaka kikao cha tarehe 15.01.2016 hakuwa ameleta barua yoyote na timu haikuleta mwakilishi kwenye kikao hicho hivyo basi kamati inaiagiza sekretarieti ya TFF kuwaandikia barua kutaka kujua ufafanuzi wa madeni ya wachezaji

i.Said Mketo anayedai Tsh 2,720,000/=

ii.Salehe Malande anayedai Tsh 2,000,000/=

iii.Rajab Isihaka anayedai kisai cha 3,720,000/= na pia kamati inataka kujua ni namna gani klabu ya Ndanda FC itawalipa wachezaji hao wanaoidai.

c. Kamati pia ilihakikishiwa na muwakilishi wa wachezaji ya kwamba wachezaji Mohamed Upatu na Amir S. Msumi waliokuwa wanaidai klabu hiyo kiasi cha Tsh 2,600,000/= kila mmoja hawaidai tena klabu hiyo na walishamalizana nao.

Snoop Dogg awaporomoshea matusi waandaaji wa tuzo za Oscar
Mtibwa Sugar Watuma Salamu Kwa African Sports