Ukarabati wa Uwanja wa CCM Kirumba, unaendelea kama Uongozi ulivyopokea maelekezo kutoka CAF kupitia Mkaguzi wa Viwanja aliyeagizwa Ndg Maxwell Mtouga
Eneo la Uwanja (Pich) ni moja ya vipaumbele vilivyoelekezwa Kuanza ukarabati, leo urejeshaji wa Udongo na Nyasi mpya kwenye maeneo ya Uwanja yaliyokuwa yameota vichuguu umekamilika, pia hatua inayofuata ni kusawazisha Udongo na Kupanda Nyasi mpya kwenye maeneo yenye Mabonde.
Pia tumepokea Trip 5 za Moramu kupitia Uongozi wa Veteran Mwanza ambao ni sehemu ya Wadau wa Uwanja wetu, Moramu hiyo itasambazwa maeneo ya Barabara ya Mbele kwenye Lango kuu la kuingilia Uwanjani
Hivyo Uongozi wa Uwanja kupitia Meneja wa Uwanja Ndg Steven E. Shija unawashukuru kwa dhati, Veterans Mwanza na Wadau wote wanaoendelea kusaidia harakati za kuuboresha uwanja wetu, ili kuufanya kuwa sehemu sahihi na Salama kwa ajiri ya Michezo na Shughuri nyingine za Kijamii, zaidi anaendelea kuwaomba wadau kusaidia kufanikisha malengo yaliyokusudiwa maana baada ya Uwanja kuwa na Viwango vya Kimataifa Jamii ya Wanamwanza na Kanda ya Ziwa itafaidika kwa namna moja ama nyingine
We Walk The Talk
Imetolewa na :-
Uongozi wa Uwanja
CCM Kirumba – Mwanza
30.03.2017