Figo ni miongoni mwa viungo muhimu vya mwili kwa binadamu kukosa kufanya kwake kazi kunaweza kusababisha magonjwa mazito na hata mauti.

Figo mwilini husaidia kutoa mkojo na uchafu wenye sumu na maji zaidi kutoka mwilini Mkojo unaotengenezwa katika figo hupitia kwenye mrija uitwao” ureta, na huteremka hadi kwenye kibofu na mwisho hutoka kupitia mrija wa urethra.

Leo nimekuandalia mambo 10 yanayoweza kuathiri utendaji kazi wa figo yako.

  1. Utumiaji vidonge vya kupunguza maumivu mara kwa mara
  2. Kubana mkojo kwa muda mrefu
  3. Mwili kukosa maji ya kutosha
  4. Kunywa pombe kali
  5. Kutumia kiwango kikubwa cha chumvi
  6. Kutumia kiwango kikubwa cha sukari
  7. Kutopata muda wa kutosha kulala usingizi
  8. Kula kiwango kingi cha protini
  9. kuvuta sigara
  10. Kunywa chai ya kahawa kupitiliza

Mfululizo wa kufanya mambo haya juu huleta madhara makubwa kwa figo, kikawaida magonjwa ya Figo yamegawanyika katika makundi mawili, kundi la kwanza ni magonjwa ya figo yanayohitaji matibabu ya kawaida na kundi la pili ni magonjwa ya figo yanayohitaji upasuaji.

Magonjwa yanayoweza kutibika ni kama Hitilafu kali ya figo, Ugonjwa sugu wa figo, Maambukizi ya mfumo wa mkojo, Hitilafu za uvimbe (nephritic syndrome).

Na magonjwa yanayohitaji upasuaji ni kama Ugonjwa wa mawe, Shida za uume, Hitilafu za kuzaliwa nazo za wa mkojo mfumo wa mkojo, Saratan.

Hivyo kuweka figo yako katika hali ya usalama inashauriwa kuepukana na mambo kumi hapo juu ambayo hudhoofisha utendaji kazi wa Figo.

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 5, 2018
Waokoaji 6 wafa maji