Watu wanatakiwa kuanza kujali ngozi zao tangu wakiwa vijana, japokuwa wengi wanajaribu kupambana na dalili za uzee pindi zinapoanza kujitokeza lakini njia pekee na salama za kuzuia kasi ya kuzeeka ni kujali ngozi yako kabla dalili hizo hazijaanza kujitokeza.
Katika mazingira tunayoishi kuna sumu na chembechembe nyingi za uchafu ambazo zina matokeo makubwa kwenye ngozi, hivyo ukitaka kujikinga kuzeeka katika umri mdogo kuna mambo unatakiwa kukaa nayo chonjo.
Maisha bora yanaweza kuchelewesha kufikia uzeni na kubadilisha muonekano wako na kufanya kuwa mwenye bora zaidi.
Hivyo leo nimekuletea tabia unazotakiwa kuachana nazo kwani tabia hizi huongeza kasi ya mtu kuzeka katika umri mdogo.
- Kutumia ”makeup” kulikopitiliza
Wanaweke wengi hutumia makeup ili kuzidi kuonekana warembo, ila kitu kikubwa ambacho watu hupuuzia ni kwamba, kutumia sana vipodozi vya kukwatua uso kuna matokeo hasi kwa afya ya ngozi yako, mabaki ya vipodozi hubakia kwenye matundu ya ngozi yako na kusababisha madhara mengi, lakini pia mabaki hayo katika matundu ya ngozi huzuia tishu kupokea oxygen ipasavyo kutokana na kuziba kwa matundu hayo.
2. Uvutaji Sigara
Sigara zina wingi wa kemikali ambayo huaribu afya na kusababisha ngozi nyororo kukomaa, sumu ya kemikali inayopatikana katika sigara huathiri mfumo wa hewa na kuingilia utengenezwaji wa tishu mpya katika mwili wako, kwa upande mwingine uvutaji sigara husabaisha mwili kupoteza kiasi kikubwa cha maji na kufanya ngozi yako kuwa kavu na iliyosinyaa hii huchagiza kasi ya ngozi yako kuanza kutengeneza mikunjo na makovu hata katika umri mdogo.
3. Kuacha kutumia vitu vinavyozuia mionzi ya jua
Kutumia vizuia mionzi ya jua kila siku inasaidia kupunguza kasi ya kuzeeka katika umri mdogo sababu bidhaa hizi zinasaidia kupunguza madhara ya miale ya jua japokuwa haitoshi kutumiwa tu wakati wa jua au ufukweni, mara zote miale ya jua hutafuta njia ya kupenyeza katika ngozi yako hivyo inasahuriwa kutumia vizuizi hivi wakati wote.
4. Kulala kwa masaa machache
Kutokulala vizuri huleta matokeo hasi kwenye ngozi yako, inashauriwa kwa siku angalau kupata masaa 7 ya kulala hivyo endapo mtu atalala chini ya masaa hayo hupatwa na uchovu ambao huchagiza ngozi kusinyaa na kujikunja kama ya mzee na macho kuchokaa.
5. Mlo usio kamili
Hii ni tabia mbaya kuliko zote inayomfanya mtu katika umri mdogo kuanza kuzeeka kabla ya umri wake, virutubisho vinavyopatikana katika chakula ni muhimu kwa kutunza afya yako na ngozi yako kuonekana nyororo na changa, hivyo kukosa mlo wenye virutubisho vyote huchagiza ngozi yako kuzeeka mapema, Utumiaji wa vyakula vingi vyenye mafuta na sukari au kutumia vyakula vingi vilivyotayarishwa viwandani hupunguza protini inayopatikana kwenye ngozi na kuongeza kasi ya kuzeeka, kwa bahati mbaya aina nyingi ya vyakula zina sumu na kemikali hatari hali mabayo husinyaisha unawiri wa ngozi.