“TUMEJIPATA.” Ni kauli ya benchi la ufundi la Tabora United likieleza kuridhishwa na kiwango cha nyota wake katika mchezo uliopita, huku likitamba kuimarika uwanja- ni na kuwapiga mkwara wapinzani michezo ijayo.

Tabora United ambao walifahamika kama Kitayosce, wanashiriki Ligi Kuu mara ya kwanza na havwakuwa na mwanzo mzuri walipocheza pungufu katika ligi na kubug- hizwa mabao 4-0 na Azam FC.

Katika mchezo uliopita dhidi ya Singida Fountain Gate walionekana kuimarika walipolazimisha suluhu ya bila kufungana na sasa wanarejea uwanja wa nyumbani kuwakaribisha Tanzania Prisons, Septemba 15.

Meneja wa timu hiyo, Rashid Hassan alisema baada ya changamoto iliyowakuta kwenye mechi ya ufunguzi, kwa sasa wamekamilika kikosini na kiwango kilichooneshwa na nyota wao dhidi ya Singida Fountain Gate kiliwapa matumaini.

“Ni kama tumejipata japokuwa bado hatujafikia malengo. Mechi mbili hatujafunga bao hata moja, lakini tunaona matumaini kutokana na kile walichokionyesha wachezaji kwenye mchezo uliopita,” alisema Hassan.

Mafuta yapaa, Wafanyabiashara wapewa angalizo
Pogba azusha kizungumkuti Juventus