Ikiwa leo ni siku ya Ukimwi Duniani, Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) imesema kuwa watu maarufu nchini hususan wasanii wako kwenye hatari zaidi ya kuambukizwa virusi vya Ukimwi.

Akizungumza na Taasisi ya Global Shappers Community Dar es Salaam, Mwenyekiti wa TACAIDS, Dk. Fatma Mrisho amesema kuwa wasanii wako katika hatari zaidi kutokana na ushawishi wao kwa umma watamaniwe na watu wengi, hivyo wanatakiwa kupewa elimu zaidi kuhusu Ukimwi.

Dk. Fatma Mrisho

Dk. Fatma Mrisho

“Watu wa muziki na burudani ni watu wenye ushawishi mkubwa sana. Wao wenyewe wapate elimu ili wajikinge kwanza halafu watoe ujumbe kwa sababu wanafuatwa sana. Ni watu ambao wana mvuto sio tu kwa vijana, hata mimi ni watu ambao nawapenda sana kwenye muziki,” alisema Dk Fatma.

Aliyekuwa Bosi wa TRA anaswa ufisadi wa Mabilioni, Magufuli Ashusha Rungu
Wakenya waandamana kupinga ufisadi, wapigwa mabomu