Serikali kupitia Tume ya Kuthibiti UKIMWI Tanzania TACAIDS imeendelea kuwekeza katika kupambana na gonjwa la UKIMWI ili kufikia malengo ya kupunguza maambukizi mpaka kufikia asilimia mbili au zero ifikapo mwaka 2030.

Akizungumza na waandishi wa Habari katika seminar iliyofanyika mkoani Morogoro Ofisa ufuatiliaji na tathmini TACAIDS Kaiser Nyangusi, Amesema kwa Tanzania UKIMWI ni gonjwa linaloongoza kuu vijana lakini pia kidunia nila pili.

Amesema kuwa Kuna sababu zinazopelekea kundi la vijana linaathirika kwa kiasi kikubwa ikiwemo kuwa na uelewa mdogo wa elimi ya UKIMWI lakini pia kufanya ngono zembe.

Amesema kundi ambalo lipo hatarini kupatwa na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ni kundi la Vijana kuanzia miaka 10 hadi 24 ambapo kundi hilo limekumbwa na ukosefu wa elimu ya kutosha kuhusu gonjwa hili hatari la UKIMWI.

Pamoja na hayo amesema kuwa hadi kufikia mwaka 2016/2017 takwimu zinaonesha asilimia 84% wanaoishi na virusi vya UKIMWI wanajitambua hali zao, kati ya hao asilimia 98% wako kwenye dawa na asilimia 92% wamefubaza virusi.

Kaimu Mkurugenzi idara ya Mwitikio wa Taifa kutoka Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Bi.Audrey Njelekela akizungumza katika Semina ya Waandishi wa Habari iliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Edema mkoani Morogoro
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Bi.Nadhifa Omar akizungumza katika Semina ya Waandishi wa Habari iliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Edema mkoani  Morogoro
Muwezesha wa Masuala ya Vijana Bi.Florence Lema akiwasilisha Mada katika Semina ya Waandishi wa Habari iliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Edema mkoani Morogoro.

Rais Samia aagiza kuu dwa kamati nyingine ya uchunguzi
Mbarawa atoa ufafanuzi daraja la Tanzanite