Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza amewatoa hofu wasanii wa sanaa ya uchoraji juu ya ufanyaji kazi wa Mradi wa Utambuzi wa Wasanii wa Sanaa za Ufundi (TACIP), ambao ulisimama kwa muda.
Akitolea ufafanuzi changamoto hiyo, alipofanya mkutano na wachoraji Jijini Dar es salaam eneo la Msasani (Tingatinga), Shonza amesema Serikali inathamini sana maendeleo ya wachoraji ndiyomaana ikatambua mradi wa TACIP ambao unasaidia wasanii wote kujulikana kwenye kanzidata na kupata manufaa mbalimbali yatatakayoboresha maisha yao.
Amesema wizara imeaza kufanyia kazi muendelezo wa mradi huo ambapo kamati maalumu iliundwa na imeshakamilisha ripoti, tayari inafanyiwa kazi na wizara ili mradi uanze kufanya kazi.
“Sisi kama Serikali tunatambua sana umuhimu wa huu mradi wa TACIP na tunajua malengo yake ambayo yalikuwa ni kukusanya kanzidata ya wasanii wote nchini Tanzania ili kwanza waweze kujulikana kisheria, lakini pili waweze kusajili kazi zao kisheria, tatu waweze kupata fursa za kuweza kukopesheka” Amesisitiza Shonza….Bofya hapa kutazama