Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania (TAFCA) kwa kushirikiana na Kampuni ya kizawa, DataVision International wanaendelea kutoa elimu kwa wasanii wa sanaa za ufundi namna gani Mradi pendwa wa TACIP utaweza kujibu changamoto zao na kuwafikisha katika daraja la maendeleo binafsi na taifa kwa ujumla. Ambapo wameanza kutoa elimu hiyo kwa wasanii waliopo Mwenge Vinyago jijini Dar es Salaam.

DataVision wameamua kutumia taaluma yeto katika kufanya tafiti pamoja na kujenga mifuno ya TEHAMA kusaidia urasimishaji wa sekta ya sanaa za Ufundi kupitia mradi wa TACIP wenye baraka za Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Mradi huo wa kihistoria umeibuliwa nchini baada ya kutambua kuwa sanaa ya ufundi ni sanaa kongwe nchini na duniani kote, lakini imekuwa haitambuliki kutokana na shughuli zake kuendeshwa bila mpangilio rasmi.

Aidha, sanaa za Tanzania zimekuwa zikiuzwa nje ya Tanzania kwa maelfu ya dola za Marekani wakati hali ya wasanii wetu inaendelea kuwa duni, ambapo hali hiyo amekuwa akiitaja Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe mara kwa mara hata katika vikao vya Bunge jijini Dodoma.

Msanii anaweza kuwa na kinyago, mathalani cha UMOJA, lakini Taasisi za Fedha hazioni kama hiyo ni dhamana inayomuwezesha kukopesheka, badalayake wamebaki na mifumo ya kale ya dhamana zisizohamishika.

Kufuatia changamoto hizo, DataVision imedhamiria kumfanya msanii na kazi zake athaminike na walau aweze kuyamudu maisha yake, kwani kazi za sanaa, kama mikeka ya kitanzania katika maeneo ya vijijini inauzwa si zaidi ya shilingi 10,000/= lakini takwimu zinaonyesha kuwa mikeka hiyo hiyo inauzwa katika masoko ya sanaa duniani kwa bei isiyopungua dola 1,000.

Hivyo, Mradi wa TACIP wenye lengo la kuwatambua wasanii utawafanya wasanii watambulike na wanufaike na kazi zao na tayari wasanii hao wameshaanza kufikiwa na kupatiwa elimu kuhusu thamani yao na jinsi mradi huo utakavyowainua.

 

Ainsley Maitland-Niles nje mwezi mmoja na nusu
Casemiro ataka ushindi wa Atletico Madrid uheshimiwe