Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imesema shehena yenye namba TCKU3337296 inayosemekana kuwa na viasili vya mionzi ya nyuklia iliyokuwa kwenye meli MV SEAGO PIRAEUS VOY 174S, ambayo inasemkana ilikuwa ikisafirishwa (Transshipment) kuja Tanzania kupitia Bandari ya Mombasa, imerejeshwa ilikotoka.

TAEC imewatoa hofu watanzania wote kuhusiana na taarifa ya tukio hilo
kwani shehena hiyo haikufika nchini.

Aidha Serikali iko macho na imejipanga vyema katika udhibiti wa uingizaji vyanzo vyote vya mionzi kupitia Bandari na sehemu zote za mipaka nchini.

Taarifa iliyotolewa na TAEC kwa vyombo vya habari imesema, iliwasiliana na Mamlaka ya Udhibiti wa Mionzi ya Nyuklia Nchini Kenya (Kenya Nuclear Regulatory Authority-KNRA) ili kubaini ukweli wa taarifa hizo ambapo KNRA ilithibitisha taarifa hizo ni za kweli, na tayari mamlaka ilichukua hatua stahiki na shehena kuamriwa kurejeshwa ilikotoka.

Pia imetoa wito kwa wafanyabiashara wote nchini kufuata sheria na
taratibu za uingizaji na utoaji wa bidhaa zao ikiwemo kupata vibali vinavyoruhusu uingizaji wa vyanzo vya mionzi na bidhaa za vyakula nchini ili kulinda na kuhakikisha usalama wa wananchi na masoko ya nje.

Simba yapokewa kwa shangwe Tabora
Sure Boy aagwa rasmi Azam FC