Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Dola kuelekea sherehe za maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanzania Disemba 9, 2021 ulinzi umeimarishwa.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Kanda Maaalum ya Dar es Salaam ACP Muliro J Muliro ametaja vikosi ambavyo vitashirikiana na jeshi la polisi kuimarisha ulinzi zaidi ni pamoja na kikosi cha upelelezi Field Force Unit FFU, Mbwa na Farasi, Polisi Marine, Polisi Reli na Polisi Main Force GD

Aidha Kamanda ACP Muliro ametoa tahadhari kwa watu watakaojihusiha na vitendo vya kihalifu kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Halikadhalika Disemba 8, 2021 majira ya satano usiku kutakuwa na milipuko salama ya fataki katika maeneo ya Uwanja wa Taifa, Daraja la Kijazi na Mnazi Mmoja kama sehemu ya sherehe ya maadhimisho ya Disemba 9, 2021.

Sambamba na hayo yote Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi wote wanaotoa taarifa mbalimbali za wahalifu na uhalifu.

Tembo Worriors watumwa kazi Uturuki
TFF: Maandalizi yanakwenda vizuri