Wananchi Mkoa wa Songwe, wametakiwa kuchukua taadhari hasa katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa mwaka, kutokana na mvua nyingi zinazonyesha kuepuka kukaa mabondeni pamoja na kuwakataza watoto kucheza na kuogelea kwenye madibwi na mito.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Theopista Mallya na kuongeza kuwa Wananchi wanapaswa pia kuwa makini ikiwa kwa sasa watoto wengi wapo mikononi mwa wazazi baada ya Shule kufungwa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Theopista Mallya.

Amesema, Wananchi kuepukana na matapeli ambao wanauza vitu kwa bei rahisi kwa lengo la la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu katika kipindi hiki cha sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya hivyo jamii imeshauriwa kununua bidhaa na kuomba risiti halali ili kujiepusha na utapeli huo.

Aidha, Kamanda Mallya pia aliwataka madereva kuongea na barabara kwa kufuata sheria za usalama barabarani na kuachana na tabia ya kuendesha gari kwa mwendokasi ikiwa ni pamoja na kuyapita magari mengine sehemu zisizoruhusiwa kwani kufanya hivyo kutapunguza ajali zinazoweza kuepukika.

Polisi waomba muda kumuhoji Bubu aliyemtupa mtoto Baharini
Picha: Waziri Mkuu awatembelea waathiriwa mafuriko Katesh