Mafuriko yaliyovunja rekodi yameikumba Pakistan tangu Juni, 2022 na kuathiri mamia ya vijiji katika sehemu kubwa ya ardhi yenye rutuba ya nchi hiyo, huku Maafisa wa Pakistan wakionya kuwa huenda ikachukua miezi mitatu hadi sita ya mvua kunyesha.
Katika Mkoa wa Sindh, upande wa kusini maji ya mafuriko yamebadilisha mashamba kuwa kama ziwa, huku Maafisa wa Pakistan wakionya kuwa huenda ikachukua miezi mitatu hadi sita, ya mafuriko kupungua.
Hadi kufikia sasa, karibu watu 1,500 wamefariki ikikadiriwa kuwa nusu yao ni watoto na zaidi ya milioni 33 wamehamishwa katika makazi yao kutokana na mafuriko, ambayo yalisababishwa na mvua kubwa ya monsuni.
Wanasayansi wanasema, ongezeko la joto duniani linaongeza kwa kasi uwezekano wa kunyesha kwa mvua kubwa katika eneo la Asia Kusini na kwamba kuyeyuka kwa barafu huchangia ongezeko la maji katika baadhi ya maeneo.
Maelfu ya watu, wamepata hifadhi katika shule na majengo ya umma au kando ya barabara, tuta za mifereji kwenye mahema ya lami na kamba, ambapo wengi wa wale ambao vijiji vyao vina unafuu wamebaki majumbani mwao, wakiwa wamezuiliwa.
Mamlaka ya Pakistani, imewataka watu kuondoka katika vijiji vilivyotengwa, na kuonya kwamba kusalia kwao kunaweza kulemea juhudi za misaada ambazo tayari zimedhoofika na kusababisha uhaba wa chakula uliopelekea maradhi ya malaria, homa ya dengue na magonjwa yatokanayo na maji.