Baadhi ya Wakulima Mkoani Arusha wamejawa na hofu kutokana na kuchipuka kwa gugu vamizi maafuru kama gugu karoti, linaloarifiwa kuathiri afya za binadamu, wanyama na shughuli za Kilimo.
Gugu hilo vamizi ‘gugu karoti’ asili yake ni Amerika Kati na linaripotiwa kuingia nchini mwaka 2010 na tayari limeenea katika mikoa mitano mpaka sasa.
Hata hivyo, mamlaka zinazohusika zinaendelea kukabiliana na tishio hilo kwa zaidi ya muongo mmoja sasa tangu kuingia rasmi mkoani humo licha ya kasi ndogo inayotumika kupambana na gugu vamizi hilo ikilinganishwa na ueneaji wake.
Miongoni mwa athari za gugu karoti ni pamoja na kupunguza ukuaji wa Mazao na kusababisha hali ya ukame na bado hakuna utafiti rasmi za kisayansi zilizofanywa nchini kuthibitisha madai ya madhara yanayosababishwa na gugu hilo.