Teknolojia inayoendelea kukua kwa kasi duniani imegeuka kuwa tishio kwa wakati mwingine hivyo mbinu mpya za ziada zinaendelea kugunduliwa katika kusaidia kuzima hatari hizo.

Maafisa wa Jeshi la Polisi nchini Uholanzi imeanza kuwafunza ndege aina ya Tai kuteka ndege zinazoruka bila rubani ambazo zimekuwa zikitanda kwa wingi kwenye anga la nchi hiyo na kuzua hali ya hatari hususan kwa ndege za abiria.

Katika mafunzo hayo, Tai wenye nguvu wanawezeshwa kupaa na kuinyakua ndege hiyo isiyokuwa na rubani na kuondoka nayo kama inavyochukua chakula.

“Tai hao wanafunzwa kuchukulia ndege hizo zisizokuwa na rubani kama mlo hivi. Hivyo, kama kawaida wanaiteka kwa haraka na kuificha mbali,” ilieleza taaria ya Jeshi la Polisi la Uholanzi.

Hata hivyo, bado kuna hatari kuwa Tai hao wanaweza kupata changamoto ya kukatwa na propela za ndege, lakini Polisi kwa kushirikiana na kampuni moja ya ulinzi ya Guard From Above, wamesema kuwa ikitokea hatari hiyo baada ya mafunzo, watawavisha nguo nzito.

Kuna idadi kubwa ya ndege zinazorushwa bila rubani nchini humo kiasi cha kuhatarisha usalama ambapo inaelezwa kuwa magaidi wanaweza kuzitumia kwa ajili ya kutekeleza dhamira zao ovu.

Aliyekamatwa akiiba mafaili ofisi ya serikali adai alitumwa na Mkuu wa Mkoa
Bungeni: Mbunge ataka serikali Ihalalishe Bangi, Mirungi.. atoa utetezi wake