Zikiwa zimepita siku chache baada ya Mahakama kuu nchini Saudi Arabia kutangaza kufutwa kwa adhabu ya viboko, Serikali ya nchi hiyo imepiga marufuku adhabu ya vifo kwa watoto.

Kamisheni ya haki za binaadamu nchini Saudi Arabia imesema serikali ya taifa hilo imepiga marufuku adhabu ya vifo kwa watoto ikiwa ni muendelezo wa hatua mpya za mabadiliko zinazotekelezwa utawala wa kifalme wa taifa hilo.

Kamisheni hiyo inasema hakuna mwenye umri mdogo, atakaekutwa na hatia, atakaepewa adhabu ya kifo, badala yake atatumikia kifungo kisichopindukia miaka 10 jela na katika gereza la watoto.

Shirika la kimataifa la utetezi wa haki za binaadamu la Amnesty International limeiweka Saudi Arabia katika orodha ya miongoni mwa mataifa yenye kunyonga watu wengi zaidi, baada ya Iran na China.

katika ripoti yake ya hivi karibuni kwa mwaka 2019 inaonesha taifa hilo limewanyonga watu 184.

Diamond kugusa kaya 500 nchi nzima, ''Anayelipa kodi milioni kayataka mwenyewe''
Watatu mbaroni kumnywesha pombe mtoto wa miaka mitatu

Comments

comments