Baada ya timu ya Taifa ya Tanzania kupata  ushindi kwa njia ya matuta dhidi ya Burundi na kuingia hatua ya makundi ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia zitakazofanyika nchini Qatar 2022 sasa Taifa Stars ina kibarua kigumu zaidi cha kukabiliana na wapinzani wengine katika michezo ijayo.

Afrika ina nchi 54 ambazo ni wanachama wa CAF nafasi za bara zima la Afrika kwenye fainali za kombe la dunia 2022 ni tano hivyo CAF imeamua kutafuta wawakilishi wake wa fainali hizo kwa kucheza mashindano katika hatua tatu.

Hatua ya kwanza ndio hii ambayo Septemba 8 mwaka huu Tanzania imewaondoa Burundi baada ya kucheza michezo miwili nyumbani na ugenini na kufanikiwa kuwatoa kwa njia ya mikwaju ya Penati 3-0 baada ya mechi zote 2 kumalizika kwa sare ya 1-1 kwa mchezo wa ugenini na 1-1 kwa mchezo wa hapa nyumbani ambapo katika hatua hii yenye timu 28 ni timu 14 tu ndio zitakazofuzu kupita.

Hatua ya pili ni ya makundi ambapo timu 26 za juu kwa viwango barani Afrika zitaungana na timu 14 zilizoanzia hatua ya awali kufanya jumla ya timu 40 ambazo zitapangwa katika makundi 10 huku kila kundi likiwa na timu nne.

Kila timu itakayoongoza kundi itakuwa imetinga hatua ya mwisho ya kutafuta watakaoliwakilisha bara letu, timu 10 zitakazokuwa zimeingia hatua hii zitacheza hatua ya mtoano nyumbani na ugenini ili kupata timu 5 zitakazokwenda Qatar 2022 kucheza fainali hizo za kombe la Dunia.

Baada ya Tanzania kuingia kwenye makundi kutakuwa na mechi sita ambazo tatu zitacheza nyumbani na tatu zitacheza ugenini tatu.

Taifa Stars ikifanikiwa kuongoza kundi ambalo wamepangiwa itakuwa imebakiwa na michezo miwili ambayo nyumbani mmoja na ugenini mmoja na kama Stars itapata matokeo bora basi itakwenda kucheza fainali za kombe la dunia 2022 nchini Qatar.

Safari bado ni ndefu hivyo watanzania waendelee kuungana na kuomba Mungu aweze kuingoza vyema ili ifike fainali, kwani ni ndoto ya kila Mtanzania kuona tunacheza kombe la dunia na mpira una matokeo na sisi tunaweza kupata matokeo mazuri.

Alichosema Ndugai juu ya uamuzi wa mahakama kesi ya Lissu
Kijana wa miaka 17 apata upofu wa macho kwa kula chips