Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Emmanuel Amunike, ametangaza kikosi cha wachezaji 30, watakaoingia kambini mwezi ujao, kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika (AFCON 2019) dhidi ya Cape Verde.

Mchezo huo wa mzunguuko wa tatu wa kundi L, umepangwa kuchezwa mjini Praia, kwenye uwanja wa taifa wa Cape Verde Oktoba 12-2018.

Kocha Amunike ametangaza kikosi hicho cha wachezaji 30, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam.

Walioitwa kuunda kikosi hicho upande wa Makipa yupo, Aishi Manula (Simba), Mohamed Abdulrahman (JKT) na Benno Kakolanya (Young Africans).

Mabeki: Shomary Kapombe (Simba), Hassan Kessy (Nkana, Zambia), Salum Kimenya (Tz Prisons), Paulo Ngalema, Ally Sonso (Lipuli) Abdi Banda (Baroka, Afrika Kusini), , Gadiel Michael, Kelvin Yondani , Andrew Vincent Dante (Young Africans) Abdallah Kheri, Agrey Morris na David Mwantika (Azam).

Viungo: Himid Mao (Pertojet, Misri), Jonas Mkude (Simba), Frank Domayo , Mudathir Yahya (Azam), Feisal Salum (Young Aficans), Saimon Msuva (El Jadidi, Morocco), Farid Mussa (CD Tenerife, Hispania), Salum Kihimbwa (Mtibwa).

Washambuliaji: Mbwana Samata (Genk, Ubelgiji), John Bocco (Simba), Thomas Ulimwengu (A Hilal, Sudani), Rashid Mandawa (BDF XI, Botswana), Yahya Zayd (Azam), Shaban Chilunda (CD Tenerife, Hispania) na Kelvin Sabato (Mtibwa Sugar)

Unai Emery akanusha kuzuia mpango wa Joachim Low
Gareth Southgate kusaini mkataba mpya