Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Abdallah Ulega ameikabidhi timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’ fedha za Posho za ndani za wachezaji pamoja na Bonasi ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Congo DRC, uliochezwa juzi Jumanne (Januari 12), Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Waziri Ulega alikabidhi pesa hizo kwa nahodha wa Taifa Stars  John Bocco, katika hafla iliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Hotel ya Tiffany jijini Dar es Salaam,  ikiwa ni sehemu ya mchango wa Serikali kusaidia maandalizi ya timu hiyo kuelekea Fainali za Mataifa Bingwa Barani Afrika CHAN 2021, zitakazounguma nchini Cameroon kuanzia Januari 16.

Waziri Ulega pia aliwakabidhi viongozi pamoja na wachezaji wa timu hiyo bendera ya Taifa.

“Serikali imechangia zaidi ya shilingi Milioni 60 kama bonasi na posho za ndani za wachezaji na benchi la ufundi, bado tunapambana kupata fedha ili kusaidia katika maeneo mengine,”

“Hakikisheni mnasimamia nidhamu ya matumizi ya fedha hizi pamoja na nidhamu kwa vijana ili timu yetu iweze kutuwakilisha vyema” alisisitiza Waziri Ulega.

Taifa Stars imeondoa leo alfajiri kuelekea nchini Cameroon kushiriki michuano ya CHAN 2021.

Taifa Stars itaanza kusaka taji la Mataifa Bingwa Barani Afrika (CHAN) kwa kucheza dhidi ya Zambia Januari 19 kwenye Uwanja wa Limbe, kicha itarejea tena dimbani Januari 23 kupepetana na Namibia na itamaliza michezo ya hatua ya makundi kwa kukutana dhidi ya Guinea Januari 27.

Senzo: Mapinduzi Cup ni kama ‘BONANZA’
Masau Bwire: Tungealikwa Zanzibar, tungetwaa ubingwa