Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania “Taifa Stars” leo kimeondoka Istanbul-Uturuki kuelekea Tunisia tayari kwa mchezo wa mzunguuko wa tatu wa kundi J wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (AFCON 2021).

Taifa Stars itacheza dhidi ya Tunisia keshokutwa Ijumaa Novemba 13 mjini Tunis, huku ikiwa na matarajio ya kupambana vilivyo na kupata matokeo mazuri.

Kwa siku tatu Taifa Stars iliweka kambi mjini Istanbul, kujiandaa na mchezo huo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini, ambao wameonyesha kukiamini kikosi cha timu hiyo.

Kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za Shirikisho la soka nchini TFF zimethibitisha kuondoka kwa kikosi cha Taifa Stars mjini Istanbul kuelekea mjini Tunis-Tunisia.

Wakati huo huo shiriksho la soka barani Afrika CAF, limetangaza orodha ya waamuzi watakaochezesha mchezo wa mzunguuko wa tatu wa kundi J kati ya Tanzania na Tunisia utakaochezwa Ijumaa Novemba 13 mjini Tunis.

Diwani afariki kabla ya kuapishwa
Magoti na mwenzake washindwa kuafikiana na DPP

Comments

comments