Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo kimepoteza alama tatu baada ya kufungwa na Lesotho 1-0, katika mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki Kombe la Mataifa Huru barani Afrika nchini Cameroon.
Taifa Stars ambayo ilikuwa ugenini, ilionesha kiwango kilichowapa matumaini Watanzania hasa katika kipindi cha kwanza, lakini makosa yaliyofanywa katika dakika ya 76, yaliwapa Lesotho goli lililotokana na mpira wa kona.
Bao 1 la Lesotho lilivyopatikana dhidi ya Taifa Stars,
Uwanja wa Tetsoto mjini Maseru, mchezo wa kufuzu Afcon. Kwa matokeo ya leo tiimu hizo zina pointi tano kila moja #MtanzaniaDigital pic.twitter.com/H8tYnGfner— Mtanzania Digital (@MtanzaniaNews) November 18, 2018
Matokeo hayo yanaiweka Tanzania katika nafasi ya nne kwenye kundi ikiwa na alama 5 sawa na Lesotho, na alama 1 mbele ya Cape Verde.
Tanzania bado inayo nafasi ingawa ni finyu zaidi kwa sasa kutokana na matokeo ya leo. Inajipanga kucheza na vinara wa kundi hilo, Uganda Cranes.
-
Waziri Mwakyembe aitaka Taifa Stars kutowaangusha Watanzania
-
Benki ya Dunia yaelezea sharti la mkopo wa elimu Tanzania
Uganda tayari wameshajipatia nafasi ya kuingia Cameroon, inaongoza kundi ikiwa na alama 13 ambazo ni zaidi ya mara mbili ya Tanzania au Lesotho.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe alihudhuria mtanange huo kuwatia moyo Taifa Stars.
Watu maarufu wametumia mitandao ya kijamii kuwatia moyo Taifa Stars kutokana na matokeo hayo, wakiwataka wajipange tena kwani nafasi bado ipo.
Kwa Watanzania na wapenzi wa soka, ninajua tumeumizwa sana na matokeo ya leo. Hata hivyo hatupaswi kuvunjika moyo kwani Bado tuna nafasi kubwa kwenda #AFCON2019. Kwa wachezaji wa #Taifastars mimi binafsi Bado nina matumaini nanyi. Mungu anataka tushindie nyumbani. Tutashinda
— Zitto Kabwe Ruyagwa (@zittokabwe) November 18, 2018