Kikosi cha Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kimerejea Dar es salaam leo Jumatatu (Oktoba 11) majira ya Alfajiri kikitokea mjini Cotonou, Benin.
Jana Jumapili (Oktoba 10) Stars ilikua na mchezo wa mzunguuko wa nne wa ‘Kundi J’ kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji wao Benin, katika Uwanja wa Taifa wa Benin (Stade de l’Amitié).
Mchezo huo ulimalizika kwa Stars kuibuka na ushindi wa bao 1-0, lililofungwa na Mshambuliaji Simon Msuva dakika 06, na kuifanya timu hiyo kuongoza msimamo wa Kundi J kwa alama saba, sawa na Binin inayoshika nafasi ya pili.
Baada ya kurejea nchini, Wachezaji wa Stars watarudi kwenye vilabu vyao kwa ajili ya kuendelea na Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/22, na mwezi Novemba wataitwa tena kwa ajili ya michezo ya Mzunguuko wa tano na sita wa ‘Kundi J’.
Stars itacheza dhidi ya DR Congo Novemba 11, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam na kisha itasafiri kuelekea Antananarivo kucheza dhidi ya Madagascar Novemba 14.