Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, kimepiga kambi mjini Tunis, Tunisia kujiandaa na mchezo wa marudiano wa kufuzu wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Algeria.

Stars itakuwa ugenini katika mchezo utakaochezwa Septemba 7, mwaka huu jijini Algers, Algeria huku ikiwa na kumbukumbu ya kukubali kichapo cha mabao 2-0, katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar es salaam.

Stars ambayo ipo kundi F, inashika nafasi ya pili katika msimamo ikiwa na Pointi saba huku Algeria ikiwa tayari imefuzu kwa kujizolea Pointi 15, Uganda ipo nafasi ya tatu ikiwa na Point nne huku Niger ikiburuza mkia na Pointi mbili.

Katika mchezo huo, Tanzania inahitaji ushindi wa Pointi tatu au sare na kujiweka katika nafasi ya kufuzu katika mashindano huo hayo.

Ofisa Habari Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Ndimbo, amesema kikosi cha wachezaji 25 kilichoitwa na Kocha Adel Amrouche, kiliondoka nchini jana Jumatano (Agosti 30).

Simba SC kupeleka mashabiki Zambia
Mapinduzi Gabon: Kiongozi wa mpito achaguliwa