Mwimbaji Tailor Swift amechangia kuweka tabasamu na pumzi kwenye uso wa mtoto Naomi Oakes mwenye umri wa miaka 11 anaesumbuliwa na ugonjwa wa leukemia kwa kuchangia kiasi cha $50,000 za matibabu na ujumbe uliogeuka faraja kuu.

Mwimbaji huyo wa ‘Bad Blood’ alitoa mchango huo baada ya kuona video inayomhusu Naomi kwenye YouTube iliyowekwa na familia ya binti huyo, Julai 5 mwaka huu.

Katika video hiyo ilieleza kuwa Naomi anasumbuliwa na leukemia na anatakiwa kupata matibabu akiwa hospitalini hapo kwa miezi sita hadi nane, hivyo angelikosa tamasha la Tailor Swift lilitakalofanyika Agosti 18, mwaka huu, Phoenix, Arizona.

Wazazi wake walieleza kuwa mbali na matibabu na ugonjwa unaomsumbua, tamasha hilo ni muhimu sana kwake kwa kuwa ni zawadi ya Christmas aliyoahidiwa na wazazi wake mwishoni mwa mwaka jana kutokana na mapenzi makubwa aliyonayo kwa Tailor.

Siku mbili baadae, mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alitoa mchango wake wa $50,000 kwa Naomi na kisha kumuandikia ujumbe mzuri akiomuomba kuvumilia na kuangalia afya yake kwanza kuliko tamasha hilo kwa kuwa bado matamasha mengine yatakuja. Kiasi hicho cha pesa kilivuka malengo ambayo wazazi wake walijiwekea katika kuomba mchango kwa watu mbalimbali.

“To the beautiful and brave Naomi, I’m sorry you have to miss it, but there will always be more concerts. Let’s focus on getting you feeling better. I’m sending the biggest hugs to you and your family,” ulisomeka ujumbe wa Tailor.
Baada ya kupata ujumbe huo, Noami alionekana kufurahi na kupata nafuu. Alieleza kuwa ujumbe huo na sapoti yake imemfanya aweze kupumua vizuri.

“I can barely breathe,” Alisema Naomi. “I seriously think I’m going to pass out right now.”
Angalia hapa Video Naomi alivyoupokea ujumbe wa Tailor Swift:

Iker Casillas Afunguliwa Milango Ya Kuondoka Hispania
Klitschko Awachokoza mabondia wa Uingereza