Rais wa klabu ya Inter Milan, Erick Thohir amethibitisha kufikia makubaliano maalum na meneja wa klabu hiyo Roberto Mancini baada ya kufanya kikao kizito hapo jana, ambacho kilitarajiwa kutoa majibu ya mustakabali ya benchi la ufundi.

Thohir amesema wamezungumza mambo mengi na Mancini, lakini kubwa ambalo lilichukua muda mrefu katika kikao chao, ni mustakabali wa majukumu aliyonayo klabuni hapo ambayo yaliripotiwa kuwa katika hatari ya kuyeyuka kutokana na kushindwa kuelewa muelekeo wake.

Tajiri huyo kutoka nchini Indonesia, amesema ameafiki kuendelea kufanya kazi na meneja huyo ambaye tangu aliporejea klabuni hapo amekua akijitahidi kusaka heshima ya The Nerazzurri.

“Roberto Mancini ni meneja wetu na ataendelea kuwepo hapa kwa sababu tumeona hakuna haja wa kutoa nafasi ya taarifa zinazozushwa dhidi yake kuendelea kuchukua nafasi katika vyombo vya habari,”

“Mkutano huu umekua na manufaa makubwa sana baina yetu, na umeleta bahati kubwa ya kuona namna ambavyo tutaweza kuboresha baadhi ya mambo, ili kufanikisha safari ya kusonga mbele,” Thohir alinukuliwa akizungumza katika televisheni ya Inter Milan

Katika hatua nyingine wawili hao wamekubaliana kusitisha mpango wa kumuweka sokoni mshambuliaji wao kutoka nchini Argentina Mauro Emanuel Icardi Rivero, ambaye alikua anahusishwa na mipango ya kuwindwa na SSC Napoli pamoja na Arsenal ya England.

“Tumekubaliana kwa pamoja suala la kuuzwa kwa Icardi halitokuwepo tena. Na ninakuthibitishia tulikua tumeshapokea ofa kutoka katika baadhi ya klabu ambazo zilionyesha nia ya kumsajili mshambuliaji huyu, lakini nichukue nafasi hii kuziarifu mpango huo hautokuwepo tena.

Wakati huo huo Thohir amethibitisha kutenga fungu la fedha za usajili ambalo litaanza kufanya kazi mara moja, kutokana na mapendekezo ambayo yamewasilishwa kwake na Mancini.

Arsene Wenger Apata Majanga Arsenal
Beppe Marotta Kuzungumza Na Wakala Wa Paul Pogba