Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa ‘TAKUKURU’ Bregedia Jenerali John Mbungo amefunguka juu ya kinachoendelea baada ya Mchezaji wa Tanzania Prisons, Benjamin Asukile kuongea hadharani na kutoa tuhuma kuwa kuna baadhi ya Viongozi wa klabu ya Young Africans kutaka kutoa Milioni 40 kama rushwa.

Asukile alitoa tuhuma hizo mara baada ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Hatua ya 16 Bora kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Young Africans, uliochezwa Ijumaa (April 30), Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga, mkoani Rukwa.

Jenerali John Mbungo amesema: “Bwana Asukile sisi tumemuita katika Ofisi zetu za Songwe na tayari wamekwisha mtumia hati ya wito kuja kueleza nini kilitokea na huo ndio wajibu wetu, tulidhani angeweza kutokea haraka lakini kwa bahati mbaya sasa hadi sasa bado hajatokea.

“Unajua watu wa tasnia ya michezo ni waongeaji kuliko watendaji. Taarifa zinakuja nyingi lakini Tunapata ushirikiano mdogo sana, niendelee kuwaalika wana tasnia wote wa michezo wajitokeze mbele kwani Ofisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa ziko Mikoani na Wiliayani kote.”

Katika mchezo wa Ijumaa, Tanzania Prisons walikubali kufungwa bao moja kwa sifuri, na kujikuta wakitupwa nje ya michuano hiyo ya Kombe la Shiriksho, ambayo sasa imeingi kwenye hatua ya Robo Fainali.

Didier Gomes afikisha siku 100 Simba
Picha 8 kutoka Kenya ziara ya Rais Samia akiwa na Kenyatta