Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) imewataka wananchi kutokaa vituoni kulinda kura baada ya kumaliza zoezi la upigaji kura, badala yake warudi majumbani.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa TAKUKURU nchini, Brigedia Jenerali John Mbung’o, wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma ambapo amesema kitendo cha kukaa kituoni kulinda kura ni viashiria vya rushwa na ni kinyume na Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa.

 “Naomba wananchi wafuate sheria wakipiga kura warudi nyumbani wasifuate maelekezo ya watu kwamba walinde kura, ” amesema Brigedia Jenerali Mbung’o. 

Aidha, Brigedia Jenerali Mbung’o amewaasa wananchi kwenda kupiga kura na kwamba ni vyema wananchi wakajiepusha na vitendo vyovyote vyenye viashiria vya rushwa kwani rushwa ni rushwa iwe ndogo au kubwa.

Kisa Ruvu Shooting, Julio amchana Ibrahim Ajib
Azam FC wakubali shughuli ya Mtibwa Sugar