Serikali imeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU, Mkoani Singida kwa kushirikiana vyama vya wafanyakazi
kuhakikisha rushwa ya ngono na unyanyasaji wa kijinsia inatokomezwa katika mkoa huo.
Rai hiyo, imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba wakati wa maadhimisho ya sherehe ya siku ya wafanyakazi kimkoa, zilizofanyika Manispaa ya Singida na kuongeza kuwa tatizo la rushwa ya ngono ni lazima likomeshwe kwenye Mkoa huo.
Kuhusu maslahi ya Wafanyakazi, Serukamba amewagiza Wakurugenzi wa Halmashauri ambao bado hawajawalipa posho watendaji wa kata kuwalipa ndani ya miezi mitatu na kutoa taarifa.
Aidha amesema, “Nichukue nafasi hii kumpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuwapandisha madaraja watumishi waliokuwa wanastahili hali ambayo imeleta motisha ndaji kazi kwa watumishi.”