Scolastica Msewa – Pwani.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU, Mkoa wa Pwani imebaini kuwa wakusanyaji wa ushuru kwenye soko la Mnarani Halmashauri ya Mji Kibaha, hawatoi risiti za mashine (EFD), baada ya Wafanyabiashara kufanya malipo, kwa kisingizio cha ubovu wa mashine.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Pwani, Christopher Myava ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kudai kuwa sababu nyingine ya kutotoa risiti hizo inadaiwa kuwa mashine hazina chaji, hali inayosababisha wakusanyaji kutumia fedha hizo kwa matumizi binafsi.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Pwani, Christopher Myava.

Aidha, amesema kutokana na hali hiyo kumepelekea kukosekana kwa kumbukumbu za wafanyabiashara waliofanya malipo, na hivyo kusababisha upotevu wa mapato.

Myava amebainisha kuwa, mradi mwingine uliobainika kuwa na changamoto ni wa mzabuni aliyechaguliwa kupeleka vifaa vya ujenzi Shule ya Sekondari ya Kata ya Shungubweni iliyopo Halmashauri ya Mkuranga, kwa kutoomba kazi hiyo kwenye mfumo wa Serikali wa TANEPS.

David Raya afichua siri nzito Arsenal
Wivu wa mapenzi wasababisha mauaji Tanga