Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU), imeeeleza kuwa imekuwa ikipokea malalamiko na kero zaidi ya 100 kwa siku nchi nzima ambazo zinahusu urejeshaji wa fedha kwa wananchi waliodhulumiwa haki zao.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa TAKUKURU Brigedia jenerali John Mbung’o kwa waandishi wa habaria imeelexa kuwa taasisi hiyo imekuwa ikitatua kero hizo ili wananchi wawe salama na mali zao, na kusisitiza wananchi wasisitite kutoa taarifa kwa sababu zinafanyiwa kazi na kutoa matokeo chanya. 

Mbali na hilo Takukuru imekanusha taarifa kwamba taasisi hiyo ya serikali  imekuwa ikiwabambikizia  wananchi kesi za tuhuma za rushwa na utakatishaji  fedha kisha kutaifisha fedha za watuhumiwa hao kutoka katika akaunti zao za benki iksema taarifa hizo ni za uongo na upotoshaji.

Mbung’o amefafanua kuwa taasisi hiyo hufanyia uchunguzi malalamiko inayopokea na unapokamilika jalada la uchunguzi  linapelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya umma (DPP)  kwa ajili ya mapitio  ya ushahidi uliokusanywa na akiridhia ushahidi, kesi inafunguliwa mahakamani.

Sambamba na hilo amesema kuelekea uchaguzi mkuu, TAKUKURU inaelimisha umma dhidi ya athari za rushwa katika uchaguzi na umuhimu wa kuchagua kiongozi mwadilifu  na mzalendo.

Watanzania zaidi ya 150,000 kufaidika na mradi wa boresha macho
Ziara ya Misri kuinufaisha Simba SC

Comments

comments