Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Taasisi ya Kupamban na Kuzuia Rushwa – TAKUKURU, Wilaya ya Tandahimba kukamilisha taarifa ya uchunguzi wa mradi ya Kituo cha Afya cha Mambamba, ambao Serikali ilitoa Shilingi 500 Milioni na bado ujenzi wake haujakamilika, ili hatua zilichukuliwa kwa wahusika.

Aidha, Njaliwa pia amewataka Watumishi wa umma nchini, kuwahudumia wananchi ipasavyo ili dhamira na maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuendelea kutoa huduma bora na kwa wakati yatimie.

Waziri Mkuu amtoa maagizo na rai hiyo wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Majaliwa Wilayani Tandahimba, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mtwara.

Amesema, “Serikali haitaki mzaha, kama wewe ni muajiriwa wa Serikali wewe ni mtumishi wa wananchi hivyo ni lazima uwahudumie. Watendaji nendeni vijijini kwa wananchi na kusikiliza kero si vema wakasubiri hadi viongozi wa kitaifa wanavyofika katika maeneo yao ndio watoe kero zao.”

Hatutarajii Wananchi kukosa Dawa Vituo vya Afya - Serikali
Viwanda: Umuhimu rasilimali Watu, Fedha wajadiliwa SADC