Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU, Mkoani Shinyanga imetakiwa kuchunguza vyama vya msingi 12 ambavyo vimeshindwa kuwalipa Wakulima zaidi ya 900 kiasi cha Shilingi bilioni 2.5.

Agizo hilo, limetolewa na Mkuu wa Mkoa huo, Chrisitina Mndeme ambapo ametoa wiki moja kwa tasisi hiyo kuhakikisha makampuni mawili ya Mkwawa na Voedsel ambayo yalifunga mkataba na wakulima kwenye ununuaji wa zao la tumbaku yaliyopitiliza miezi minne bila kuwalipa wakulima.

Amesema, “Vyama hivyo ni Kangeme, Kasela, Mbuni, Twiga Mapamba, Mihama Kabanga Mtakuja Iringabalimi, Nyakashatara, Kimumwe vimeshindwa kurejesha fedha kwenye mabenki kwa asilimia 100 waliyokopa nakushindwa kuwalipa wakulima.”

“Atakaye bainika kusababisha hasara hiyo achukuliwe hatua ya kufikishwa mahakamani na hakuna chama kitakachoanzishwa kipya bali vyama hivyo vifufuliwe upya hatuwezi kukubali Sh biloni 2.5 zipotee bure,”alisema Mndeme.

Aidha, alisema kampuni ya Mkwawa na Voedsel wanazonunua tumbaku alitaka kufikia Septemba 22, 2023 iwe mwisho wawe wamekwisha walipa wakulima wote kwa asilimia 100 kiasi wanachodai zaidi ya dola Millioni 9.5.

Mndeme alisema zao la tumbaku msimu wa 2022/2023 wamefanikiwa kuuza na kuzalisha zaidi ya kilo Millioni 14.38 yenye thamani zaidi ya Sh bilioni 90 na kutaka mkataba wa wakulima na makampuni baadhi ya vipengele viangaliwe upya ili mkulima anufaike.

Kwa upande wake Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoani Shinyanga Hilda Boniface alisema vyama 12 vinadaiwa na mabenki nakusababisha vyama hivyo kufa kutokana na kutokopesheka tena pia wapo wakulima wanadai kwenye makampuni ambayo wameyauzia tumbaku.

“Changamoto iliyokuwepo wakulima kwenye vyama hivyo wamekuwa wakitorosha tumbaku kwenda kujisajili kwenye vyama vingine ambavyo havidaiwi nakubadili jina huku deni la vyama walivyotoka linakuwa palepale, ”alisema Boniface.

Ntibazonkiza aweka rekodi mpya CAF
Kiza kinene suluhu mgomo wa nyongeza ya Mshahara