Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) kimempongeza Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini, Joseph Kasheku maarufu kwa jina la Msukuma kwa kulivalia njuga suala la watumishi wa umma waliofukuzwa kazi hatimaye kurudishwa kazini.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa chama hicho, Rashid Mohamed Mtima alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

“Suala hili sisi tumeanza muda mrefu kulihangaikia lakini, wiki iliyopita tuliwaona wabunge walivyokuwa wamechachamaa Bungeni wakiongozwa na Mbunge wa jimbo la Geita Mjini, Joseph Kasheku Msukuma kwa kuweza kulipigia kelele jambo hili tunawashukuru sana,”amesema Mtima

Aidha, amesema kuwa kwa niaba ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU), ameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuzingatia mapendekezo waliyowasilisha serikalini Machi 22, 2018 na hatimaye kufanyiwa kazi.

Hata hivyo, Mtima ameongeza kuwa wanachama wake wamefurahishwa na uamuzi huo wa serikali kwa kuwa umeweza kurudisha matumaini mapya kwa watumishi hao waliofukuzwa kazi hapo awali.

 

 

 

Trump achukizwa na kitendo cha FBI kupekua ofisi za Cohen
Mwanamke aliyewapa wenzake mimba feki afungwa jela