Wajumbe wa Taliban leo Januari 24, 2022 wanakutana na maafisa wa nchi za magharibi nchini Norway kwa ajili ya mazungumzo ya kwanza Ulaya tangu kundi hilo lichukue udhibiti wa nchi ya Afghanstan.
Mazungumzo hayo, yaliyopangwa kufanyika kwa muda wa siku tatu, yatakijita katika suala la haki za binadamu pamoja na mzozo wa kibinadamu katika nchi hiyo, ikiwa leo ni siku ya pili baada ya kukukata siku ya jumapili.
Aidha inasemekana kuwa leo ni siku muhimu ya mazungumzo baina ya wajumbe wa Taliban na maafisa wa magharib. Kikundi hicho kimepanga kuomba kupata mabilioni yake ya dola yaliyofujwa katika benki za Marekani.
Umoja wa Mataifa unasema 95% ya Waafghanstan hawana chakula cha kutosha, huku maandamano kadhaa yamefanyika Ulaya huku wakosoaji wakidai kuwa Taliban haipaswi kuzawadiwa kwa mazungumzo.
Afghanistan imeshuhudia ukosefu wa ajira na mfumuko wa bei za bidhaa, huku thamani yasarafu yake ikiporomoka na benki zimeweka ukomo wa kiasi cha pesa ambazo zinaweza kutolewa kwenye akaunti ya benki.