Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wametoa tamko lao baada ya jeshi la polisi kuzuia kongamano lililotakiwa kufanyika kumuenzi aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho, Alphonce Mawazo mkoani Geita.
Mmoja wa wanachama wa Chadema, Dr. Mussa Mdede ambaye pia katika kongamano hilo alikuwa mmoja kati ya watoa mada, amesema kitendo hiko cha polisi kuzuia Kongamano ni kitendo kinyume na sheria Namba 5 ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 1995.
”Jeshi la polisi linahitajika kuimarisha ulinzi na usalama kwenye mikutano ya hadhara ndivyo sheria inavyosema”. amesema Mdede.
” Kongamano ambalo limezuiwa ni shughuli ya ndani ambayo kimsingi sheria ya vyama vya siasa inatulinda. Kimsingi ni kongamano ambalo lilikuwa halali na tunapofanya kongamano la ndani hatuhitaji ulinzii wa jeshi la polisi” amesema Mussa Mdede.
Hivyo Mdede amemuomba mkuu wa jeshi la polisi nchini, IGP Sim0n Sirro kutumia nafasi yake kuwakumbusha polisi majukumu yao kwani kwa sasa anaona wanafanya kazi kwa mwamko wa kisiasa.
Chadema tunasema, kwanza tunamwambia IGP Simon Sirro kwamba awakumbushe Askari wake kufanya kazi kwa weledi wasifanye kazi kwa kisiasa. Katika awamu hii ya tano jeshi la polisi limekuwa likifanya siasa waziwazi.” Mussa Mdede.