Mkurugenzi Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania, (TAMWA), Rose Reuben amesema kuwa amefurahishwa na uteuzi uliofanyawa na Rais John Magufuli, kwani umezingatia usawa wa kijinsia.

Kwa mujibu wa East Africa Radio, Rose amesema uteuzi wa Rais Magufuli, unadhihirisha kuwa yale yote waliyokuwa wanasema kuhusiana na wanawake yalikuwa mambo ya msingi.

“Nimeufurahia uteuzi wa Rais John Magufuli kwasababu umeweza kukumbuka na kuelewa yale tuliyokuwa tukishawishi kwamba  upo umuhimu wa kuwaweka wanawake katika ngazi mbalimbali” amesema Rose Reuben.

Kauli ya mkurugenzi wa TAMWA inafuatia baada ya uteuzi wa Rais Magufuli siku ya jana ambapo aliwateua Bi. Riziki Said Lulida na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi (CCM),Humphrey Polepole, kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

UN yakanusha idadi ndogo waliouawa Nigeria
Kiswahili kuanza kutumika katika shule Afrika Kusini

Comments

comments